JE!
NAWEZA KULIPATA KANISA Mara kwa mara Mungu ametoa ujumbe wa pekee kukidhi mahitaji ya vizazi tofauti mbali mbali: ujumbe wa kumsaidia Adamu na Hawa baada ya dhambi kuiharibu dunia yao, ujumbe kwa ulimwengu uliokuwako kabla ya gharika ile kuu ya maji, ujumbe kwa Israeli wakati Ashuru au Babeli ilipowatishia. Yesu alikuja na ujumbe maalum kwa siku zetu. Sura ya 12 na 14 ya Ufunuo hutoa muhtasari wa ujumbe wa Mungu wa pekee kwa ajili yetu leo. Katika GUNDUA Mwongozo huu na mwongozo ule unaofuata, tutauangalia ujumbe huo. 1. Kanisa Lilianzishwa Na Yesu Maisha
na mafundisho ya Yesu yalianzisha umoja wa imani na ushirika wa karibu
sana katika kanisa lile la mitume walilolianzisha. Mitume wale walikuwa
na uhusiano wa karibu kabisa na Kristo yule aliyefufuka. Paulo alitoa
picha ya kifungo hicho cha karibu sana na kukilinganisha na uhusiano
wa ndoa: Kulingana na maneno ya Paulo, kanisa la Kikrsto ni mwanamke safi, ni bibi-arusi wa Kristo, ishara inayofaa kabisa kwa kanisa lake Kristo alipendalo. Katika Agano la Kale mithali iyo hiyo inatumika kuielezea Israeli, yaani, wateule wa Mungu. Mungu aliwaambia Israeli: "wewe kama bibi-arusi ulinipenda mimi" (Yeremia 2:2); "Mimi ni mume wenu" (Yeremia 3:14). Kitabu
cha Ufunuo pia kinazungumza juu ya kanisa kama mwanamke: Mwanamke huyo ame"vikwa jua". Maneno hayo yanadokeza kanisa linalong'aa kama jua, kwa sababu ya kuvikwa utukufu wa kuwako kwake Kristo. Yesu, "Nuru ya Ulimwengu" (Yohana 8:12), anaangaza kupitia kwa washiriki wa kanisa lake, nao kwa upande wao wanapaswa kuwa "nuru ya ulimwengu" (Mathayo 5:14). Mwanamke huyo ana"mwezi chini ya miguu yake." Mwezi huo unawakilisha nuru ya Injili iliyoakisiwa [iliyoangaza] katika dhabihu na taratibu za ibada ya watu wa Mungu katika Agano la Kale. Mwezi huo ukiwa "chini ya miguu yake" unadokeza kwamba nuru ya Injili iliyoakisiwa imepitwa na huduma anayofanya Kristo. Mwanamke huyo anayo "taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake." Nyota zinawakilisha vizuri sana mitume wale kumi na wawili, watu waadilifu ambao ushuhuda wao juu ya Yesu unang'aa sana mpaka siku hii ya leo. Ni dhahiri, basi, kwamba maelezo yamhusuyo mwanamke huyo yanaonyesha kwamba Yohana katika mawazo yake analiona badiliko lililotokea kutoka kwa watu wa Mungu, Israeli, katika Agano la Kale kwenda kwenye kanisa lile la Kikrsto la Agano Jipya alilolianzisha Yesu. Jua, mwezi, na nyota huitilia mkazo huduma ya kupeleka nuru inayofanywa na kanisa hilo la Kikristo kwa kuzitangaza hizo Habari Njema. 2. Matukio Yanayofuatana Ya Kushindwa Kwa Shetani Kuingia
kwa mwanamke huyo kunaweka jukwaa kwa matukio haya makuu yanayofuatana:
Wakuu
watatu wanashiriki katika mfululizo wa matukio haya: Picha hiyo inakuwa dhahiri mara tu tunapoifahamu mifano hiyo. Ibilisi na malaika zake "wa[lipo] poteza mahali pao mbinguni," wali"tupwa duniani." Yesu alipozaliwa katika dunia hii, Ibilisi alijaribu kumwua Yesu, mwana yule wa kiume, mara tu alipokwisha kuzaliwa. Alishindwa, kisha Yesu "akanyakuliwa" kwenda kwenye kiti cha enzi cha Mungu. Ndipo
Shetani akaondoka kwenda kuliangamiza kabisa kanisa la Kristo alilolianzisha
Kristo. Mtume Yohana, aliyekiandika kitabu cha Ufunuo, aliliona kidogo
tu pambano hilo kuu kati ya Kristo na Shetani likipiganwa vikali sana
juu ya dunia hii. Vita hiyo ilipofikia kilele chake wakati ule wa kusulibiwa
kwake Kristo, Yohana alisikia sauti ikipiga kelele kutoka mbinguni,
ikisema: Yesu alipata ushindi dhidi ya Shetani pale msalabani. Wakati ule ndipo alipothibitisha uhakika wa mpango ule wa "wokovu" na kutoa "uwezo" wa kuzipinga hila za Shetani. "Ufalme wa Mungu" ukaimarishwa, na "mamlaka" ya Mwokozi ya kuwa Kuhani wetu Mkuu na Mfalme wetu ikawa imethibitishwa. "Sasa umekuja wokovu" ni tangazo linaloonyesha kwamba tendo lile la kilele la historia limefika. Kuzaliwa kwake Kristo, Mwokozi wa ulimwengu, kumekwisha kutokea (fungu la 5). Licha ya majaribu makali ya Shetani, Yesu aliishi maisha yasiyo na dhambi, alikufa na kufufuka akiwa mshindi dhidi ya dhambi na mauti (fungu la 10). Shetani ameshindwa milele (fungu la 7-9). Msalaba umetukuzwa katika uwezo wake wote. Tangazo
hili, "Sasa umekuja wokovu," halimpendezi Yohana tu, bali
malimwengu yote: Mbingu yote ilisherehekea ushindi wa Kristo. Kristo aliyavunjilia mbali madai ya aina yo yote ile aliyokuwa nayo Shetani zamani kuhusu kuwa na mahali pake kule mbinguni, na yule Shetani aliyeshindwa akapoteza milele madai yake aliyosema dunia hii ni yake. 3. Kanisa La Kikristo Katika Mapambano Dhidi Ya Shetani Kabla Yesu hajapaa kwenda mbinguni alilianzisha kanisa la Kikristo (ambalo linafananishwa na mwanamke). Kifo chake pale msalabani kililipa hilo kanisa la Kikristo uwezo wa kumshinda Shetani. "Nao [Kanisa la Kikristo] wakamshinda [Shetani] kwa damu ya Mwana-Kondoo na kwa neno la ushuhuda wao; hawakuyapenda sana maisha yao kiasi cha kuogopa kufa." - (Ufunuo 12:11). Kristo
anaweza kulipa kanisa lake uwezo wake sasa, yaani, kulipa lile tunda
la ushindi wake. Yesu alimshinda Shetani kabisa kwa njia ya kanisa lake.
Sifa tatu zinalitambulisha kanisa hilo lenye kushinda katika karne zilizokuwa
zikiendelea kupita za kipindi hiki cha Kikristo: Ufunuo 12:11 huonyesha picha ya kanisa linaloshinda ambalo limejaa washindi: mitume, wafia dini, wanamatengenezo ya kanisa, na Wakristo wengineo waaminifu. Upole, uaminifu, ujasiri, na ushindi wao umenguruma kushuka katika karne nyingi na kuupindua ulimwengu. Kwa kuwa Shetani alishindwa kumwangamiza Yesu alipoishi hapa duniani, sasa anajitahidi sana kumwangamiza Kristo anayeishi ndani ya kanisa lake. "Joka lilipotambua kwamba limetupwa chini duniani, likaanza kumwinda yule mama aliyekuwa amejifungua mtoto wa kiume. Lakini mama huyo akapewa mabawa mawili ya tai apate kuruka mbali sana na hilo joka, mpaka mahali pake jangwani ambapo angehifadhiwa salama kwa muda wa miaka mitatu na nusu. Basi, joka likatapika maji mengi kama mto, yakamfuata huyo mama nyuma ili yamchukue. Lakini nchi ikamsaidia huyo mama: ikajifunua kama mdomo na kuyamezaaa maji hayo yaliyotoka kinywani mwa hilo joka - (Ufunuo 12:13-16). Kama vile ilivyotabiriwa, katika zama zile za giza za kipindi kile cha Kikristo, Shetani alitoa "mto" wa mateso ili kufanya kanisa li"chukuliwe na mkondo ule wa mto." Shetani anataka kuufutilia mbali mvuto wa Kristo kwa kulifutilia mbali kanisa lake, tena anatumia kila hila ambayo akili yake nyingi iliyojaa uovu inaweza kubuni. Kimsingi Joka anamwakilisha Shetani. Lakini kumbuka kwamba Shetani anazitumia taasisi za wanadamu katika utendaji wake kama joka ili kuwashambulia watu wa Mungu. Alimtumia mfalme wa Kiroma Herode katika jaribio lake la kumwua mtoto Kristo mara tu alipokwisha kuzaliwa. Alifanya kazi yake kupitia kwa viongozi wa dini wenye husuda na wenye kuwania madaraka waliomnyemelea na kumsumbua Mwokozi, na hatimaye kumwua juu ya ule msalaba. Lakini ule ulionekana kama ni ushindi mkubwa usio na kifani wa Kristo. Akiwa amekasirika vibaya sana dhidi ya kushindwa kwake pale msalabani, Shetani akaielekeza ghadhabu yake dhidi ya Kanisa lile alilolianzisha Yesu. Katika miongo [miaka kumi-kumi] iliyofuata baada ya kusulibiwa kwake Kristo, maelfu waliuawa katika ule uwanja wa duara uliojengwa mjini Roma (Colosseum), maeneo tupu ya pembe mraba yaliyokuwa mijini, magereza yale ya chini ya ardhi, na katika maficho ya jangwani. Mwanzoni wale wenye mamlaka [serikali] ya kidunia walianzisha hayo mateso. Lakini baada ya kufa wale mitume badiliko lilitokea taratibu ndani ya kanisa lile. Katika kipindi kile cha karne ya pili, ya tatu, na ya nne, wengi ndani ya kanisa lile walianza kuzibadili kidogo zile kweli zilizokuwa zimefundishwa na Kristo pamoja na mitume wake. Viongozi fulani, walioasi hata wakaanza kuwatesa Wakristo wale waliosisitiza kuwa na usafi wa itikadi [imani] za Agano Jipya. Wataalam wa Biblia wanakadiria kwamba takriban milioni 50 ya wale waliokuwa waaminifu waliuawa. Katika jitihada yake ya kulizamisha na kuliangamiza kanisa, Ibilisi alitoa "mto" wa mateso ili kulifanya "lichukuliwe [lile kanisa] na mkondo ule wa mto." "Lakini nchi ikamsaidia yule mwanamke kwa kuumeza ule mto" wa mateso na mafundisho ya uongo. Katika kipindi cha mateso ya Zama za Kati [1100-1500], kanisa la kweli lilijiondoa kutoka katika uongozi ule ulioasi na kujificha "Nyikani, mahali alipoandaliwa na Mungu, ili wamlishe muda wa siku 1,260" (fungu la 6). Utabiri huo ulitimizwa katika kipindi cha miaka 1260 ya mateso kuanzia mwaka wa 538 hadi mwaka wa 1798 B.K. (siku moja mara nyingi husimama badala ya mwaka mmoja katika unabii wa mifano wa Biblia, angalia Ezekieli 4:6). Katika kipindi cha karne za giza Wakristo waaminifu walioiamini Biblia walipata kimbilio lao po pote walipoweza kupapata kwa mfano, katika mabonde ya Wawaldensia wa Italia magharibi na Ufaransa mashariki, na katika kanisa la Kikeltiki [Waskoti Waairishi, Waweishi] la visiwa vya Uingereza. 4. Kanisa La Mungu Katika Siku Hizi Zetu Jambo hilo linatufikisha katika siku hizi zetu - yaani, kwenye kanisa la kweli la Kristo tangu mwaka wa 1798. Kama ambavyo ingeweza kutarajiwa, yule joka bado amewakasirikia watu wa Mungu. Vita kuu isiyoonekana kwa macho inaendelea. Kwa kweli, Shetani anafanya shambulio lake kubwa kabisa dhidi ya kanisa hilo muda mfupi tu kabla ya kuja kwake Yesu. "Ndipo yule Joka [Ibilisi] akamkasirikia sana yule mwanamke [Kanisa la Mungu], akaenda zake afanye vita dhidi ya wazao wake waliosalia - wale wanaozitii amri za Mungu na kuwa na ushuhuda wa Yesu." - (Ufunuo 12:17). Unabii
huu unalenga katika siku zetu hizi. Shetani amekasirika sana; anafanya
vita dhidi ya wazao wa mwanamke waliosalia" - yaani, dhidi ya watu
wa Mungu wa siku hizi. Angalia alama zao zinazowatambulisha: (2) Wakristo hao wa siku za mwisho ni watu wa unabii. Kuupokea ule "ushuhuda wa Yesu Kristo" kulimwezesha Yohana kukiandika kitabu kile cha Ufunuo (Ufunuo 1:1-3). Kundi hilo la mwisho la waumini linapokea karama ile ile: yaani, ushuhuda wa moja kwa moja toka kwa Mungu kupitia kwa mjumbe wa kibinadamu. Karama yao ya unabii inalenga juu ya ufunuo wa Mungu kuhusu utume wao na mwisho wao. (3) Wakristo hao wa siku hizi za mwisho wanatambulikana pia kama "wale wanaozitii Amri [kumi] za Mungu." Hawatetei tu ukamilifu wa hizo Amri Kumi, bali wanazitii pia. Upendo wa Mugu ulio mioyoni mwao unawaletea utii unaotolewa kwa moyo wa furaha (Warumi 5:5; 13:8-10). Wakristo
hao wa siku hizi za mwisho wanakifuata kielelezo cha Kristo na cha kanisa
lile la kwanza kwa kuzitii amri [kumi] za Mungu. Jambo hilo linamkasirisha
vibaya sana yule Joka - yaani, yule Ibilisi. Naye anapigana vita dhidi
ya "wazao" wa mwanamke "waliosalia" kwa sababu wanatoa
ushuhuda kwamba upendo wao kwa Mungu unawafanya wafuasi wake hao kuwa
watii. Kama vile Kristo alivyoagiza, aliposema: Maisha ya Wakristo hao wa siku hizi za mwisho yanaonyesha kwamba uwezekano upo wa kumpenda Mungu kwa mioyo yetu yote na kuwapenda wenzetu kama sisi tunavyojipenda wenyewe. Kulingana na maneno ya Yesu, sifa hizo za tabia, yaani, upendo kwa Mungu na upendo kwa watu, hufanya muhtasari wa Amri kumi za Mungu (Mathayo 22:35-40). Ya nne katika hizo amri inatutaka sisi kuitunza Jumamosi, siku ya saba ya juma, kama Sabato. Kwa kuwa upendo wao kwa Yesu umezitia ndani ya mioyo yao amri zote kumi [Ebr. 8:10; Kut. 20:3-17; Yak. 2:10-12], basi, Wakristo hao wa siku hizi za mwisho ni Wasabato. Sabato ndicho kiini cha ujumbe wa mwisho wa Mungu kwa watu wake katika kitabu cha Ufunuo, sura ya 12 na 14:6-15. Nguvu zote za mbinguni zinajipanga nyuma ya Wakristo hao wa siku hizi za mwisho walioelezwa katika sura hizo. Mwokozi wao aliye hai ndiye rafiki yao daima, na Roho Mtakatifu anafanya kazi yake "kuwafanya imara kwa nguvu katika utu wao wa ndani." Ahadi yake ni ya hakika. WATAmshinda Shetani "kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao" (Ufunuo 12:11). Je! unataka kuwa mmoja wa Wakristo hao wa siku hizi za mwisho ambao "wanazitii amri [kumi] za Mungu" tena wa"na ushuhuda wa Yesu"? Kwa nini usikate shauri sasa hivi?
© 2004 The
Voice of Prophecy Radio Broadcast | |