![]() |
![]() |
||||||||||||||||||||||||||
![]() |
![]() |
JE! MUNGU ANA HAKI?
Mama mmoja kijana katika viunga vya mji anagundua kwamba mtoto wake amepatikana na Ukimwi kutokana na damu aliyoongezewa mwilini mwake. Misiba inazidi kuendelea tena na tena katika ulimwengu wetu huu. Nasi tunatamani sana kujua jibu kwa mambo hayo yote. Hivi Mungu huyo yuko wapi katika ulimwengu wetu huu uliojaa mateso na vifo visivyo na maana? Mtunga Zaburi anatuhakikishia sasa kwamba " dunia hii imejaa upendo wake usio na mwisho" (Zaburi 33:5). Lakini, basi, kama hilo ni jambo la kweli, mbona hayakomeshi mateso hayo pamoja na misiba? Sura ya 20 ya Ufunuo inatuonyesha sisi ni kwa ajili gani na lini Mungu atakapo komesha dhambi na mateso. 1. Miaka Ile Elfu Moja Yafunuliwa Ufunuo 20 huelekeza mawazo yetu yote kwenye kipindi kile cha miaka 1,000 ambacho kinakuja baada ya Kristo kuja mara ya pili. Matukio yale yanayokizunguka kipindi hicho cha mika 1,000 ni lile tendo la mwisho katika pambano ambalo limekuwa likiendelea kati ya Kristo na Shetani tangu dhambi ilipoingia katika ulimwengu huu.
Je!
Ni akina nani hao ambao Mungu anawafufua kutoka kwa wafu katika ufufuo
wa kwanza unaotokea mwanzo wa ile miaka 1,000? Wale walio "heri na watakatifu," yaani, wale waliompokea Kristo kama Mwokozi wao wanatoka katika ule ufufuo wa kwanza wa wenye haki na hawana budi kutawala pamoja na Kristo katika kipindi cha miaka 1,000 basi, ni lazima wafufuliwe mwanzo wa ile miaka 1,000. Je hao ni akina nani wanaofufuliwa katika ufufuo wa pili utakaotokea mwisho wa kipindi cha miaka elfu moja? Hao wafu Waliosalia hawakuwa hai mpaka ilipokwisha ile miaka elfu moja - (Ufunuo20:5). Maneno haya "hao wafu waliosalia" yanaweza tu kuwataja waovu wale waliokufa kwa sababu wale wenye haki ambao ni heri na watakatifu wanaofufuliwa mwanzo wa ile miaka 1000. Kwa hiyo, hicho kipindi cha miaka 1,000 kimetenganishwa na ufufuo wa aina mbali : yaani, ufufuo wa wenye haki unatokea mwanzo wake, na ufufuo wa waovu unaotokea mwisho wake. 2. Kufufuliwa Wakati Wa Marejeo Ya Kristo Ufufuo wa kwanza, yaani, ule wa wenye haki unatokea wakati wa kuja mara ya pili kwa Kristo.
Yesu anapokuja katika dunia hii anawafufua wale "waliokufa katika Kristo" na kuwachukua kwenda nao mbinguni pamoja na wenye haki wale walio hai. Kwa kuwa wale waovu bado wanaendelea kung'a ng'ania dhambi, hawawezi kuendelea kuwa hai mbele zake Mungu, nao wanaangamizwa wakati ule wa kuja kwake Kristo (Luka 17:26-30). (Unaweza kupenda kupitia tena Mwongozo 8 uhusuo matokeo yale yanayoambatana na kurudi kwa Yesu). 3.
Shetani Afungwa Mnyororo Hapa Duniani Kwa Miaka Elfu Moja "Kisha, nikamwona malaika mmoja anashuka kutoka mbinguni akiwa na ufunguo wa kuzimu na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Akalikamata lile joka - nyoka wa kale, yaani Ibilisi au Shetani - akalifunga kwa muda wa miaka elfu moja. Malaika akalitupa kuzimu, akaufunga mlango wa kuingilia huko na kuutia mhuri ili lisiweze tena kuyapotosha mataifa mpaka hapo miaka elfu moja itakapotimia. Lakini baada ya miaka hiyo ni lazima lifunguliwe tena, lakini kwa muda mfupi tu " Ufunuo 20:1-3.
4. Wenye Haki Wanawahukumu Waovu Kipindi kile cha miaka elfu moja ni kipindi cha hukumu pia. Lakini kumbuka kwamba hukumu hiyo ina hatua kuu nne: (1)
Hukumu ya wenye haki kabla ya kuja kwa Kristo mara ya pili. Tumekwisha kuona ya kwamba wenye haki waliokufa ambao wamekwisha kufufuliwa, pamoja na wenye haki wale walio hai wananyakuliwa kwenda mbinguni wakati ule wa kuja kwake Kriso mara ya pili. Wao wako nyumbani kwao kule mbinguni katika kipindi kile cha miaka 1,000. Je, watakuwa wakifanya nini huko? "Je! hamjui kwamba watu wa Mungu watauhukumu ulimwengu? Ikiwa basi, ulimwengu utahukumiwa nanyi kwa nini hamstahili kuhukumu hata katika mambo madogo? hamjui kwamba, licha ya kuhukumu mambo ya kawaida ya kila siku, tutawahukumu hata malaika?" - (1 Wakorintho 6:2-3). "Kisha nikaona viti vya enzi na watu walioketi juu yake; watu hao walipewa mamlaka ya hukumu. Niliona pia roho za wale waliokuwa wamenyongwa kwa sababu ya kumshuhudia Yesu na kwa sababu ya neno la Mungu. hawa hawakumwabudu yule mnyama na sanamu yake, wala hawakupigwa alama yake juu ya paji ya nyuso zao, au juu ya mikono yao. Walipata tena uhai, wakawatawala pamoja na Kristo kwa miaka elfu moja "- (Ufunuo 20:4).
Kwa neema yake nyingi Mungu amewapa wanadamu waliokombolewa nafasi ya kutathmini alivyowashughulikia waovu. Tunaweza kuwa na maswali mengi kama haya: "mbona shangazi yangu hayupo hapa? Alionekana kana kwamba alikuwa mtu mzuri" Tutakapozipitia kumbukumbu zile na kuwahukumu wale wafu " kulingana na matendo yao kama yalivyoandikwa katika vitabu vile" (fungu la 12), tutajionea wenyewe ya kwamba katika kushughulika kwake kote kule na wanadamu, Mungu amekuwa wa haki wala hana upendeleo kwa kila mtu. Tutaona jinsi Roho Mtakatifu alivyowapa wanadamu nafasi baada ya nafasi ili wapate kujitoa kabisa kwa Mungu, na haki ya kila hukumu itaonekana wazi. 5. Shetani Afunguliwa Mwisho Wa Ile Miaka Elfu Moja Mwisho
wa ile miaka 1,000 Biblia inatangaza hivi: Mji huu wa ajabu umekuwa makao yetu kwa miaka elfu moja. Sasa Mji huu Mtakatifu - ndani yake ukiwa na Kristo na watu wote aliowakomboa - unashuka kutoka mbinguni kuja katika dunia mpya. Je! Shetani anafanya nini mwisho wa mika hiyo 1,000? "Wakati miaka elfu moja itakapotimia, Shetani atafunguliwa kutoka gerezani mwake. Basi, atatoka nje, ataanza kuyapotosha mataifa yote yaliotawanyika kila mahali duniani, yaani Gogu na magogu. Shetani atawakusanya pamoja kwa ajili ya vita; nao watakuwa wengi kama mchanga wa pwani. Walipita katika nchi yote, wakaizunguka kambi ya watakatifu na mji wa Mungu aupendao. Lakini moto ulishuka kutoka mbinguni, ukawaangamiza" - (Ufunuo 20: 7-9).
6. Mandhari Ya Hukumu Ya Mwisho Hapo, kwa mara ya kwanza, wanadamu wote wanakutana pamoja ana kwa ana. Yesu anawaongoza wana wa Mungu waliokombolewa ambao wamo ndani ya mji huo. Shetani anaongoza akiwa mbele ya hilo kundi kubwa sana lililosongamana la waovu ambao wako nje ya kuta hizo. Katika wakati huu wa hatari sana, Mungu anatekeleza hatua ya mwisho ya hukumu na waovu wanapokea siku yao katika mahakama hiyo. "Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yule aketiye juu yake. Dunia na mbingu vikatoweka mbele ya macho yake, na havikuonekana tena. Kisha nikawaona watu wakubwa na wadogo, wamesimama mbele ya kiti cha enzi, na vitabu vikafunguliwa. Halafu kitabu kingine, yaani kitabu cha uhai, kikafunguluwa pia. Wafu wakahukumiwa kadri ya matendo yao, kama ilivyoandikwa ndani ya vitabu hivyo" - (Ufunuo 20:11,12). Waovu wanaposimama mbele ya hicho kiti cha enzi cha hukumu, maisha yao yote yanaonyeshwa mbele yao. Kutoka katika zile kumbukumbu zilizoko kule mbinguni, Yesu, Jaji mwenye haki, anakifunua rasmi kisa chake kamili kuhusu jinsi alivyowashughulikia wanaume, wanawake, na malaika walioanguka.
"Sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu. Imeandikwa: 'Kama niishivyo,' asema Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu; na kila ulimi utamkiri Mungu!" - (Warumi 14:10-11). "Kristo Yesu akawa mtii hata mauti - naam, mauti ya msalaba!. Ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, mbinguni na duniani.. kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba" - (Wafilipi 2:5-11). Tangu dhambi ilipoanza, Ibilisi amekuwa akiielezea vibaya tabia ya Mungu, akimshtaki kwamba hatendi haki. Lakini sasa maswali yote yamejibiwa, utata wote umeondolewa. Sasa kila kiumbe aliye katika hayo malimwengu anakiri kwamba Yesu, Mwana-Kondoo wa Mungu, anastahili kupewa upendo wetu na kuabudiwa. Mpango wote na kusudi la Mungu sasa vimefunuliwa kikamilifu, na tabia ya Mungu inasimama ikiwa imethibitishwa kuwa ni ya haki. Si wale tu waliokombolewa, bali pia wale malaika waovu pamoja na Shetani mwenyewe watakiri kwamba njia ya Shetani imekuwa na makosa na ya kwamba njia za Mungu ni za haki na za kweli. Wote wanaona wazi kwamba uovu na uchoyo vimeleta huzuni tu na kutokuridhika, na kwamba mambo hayo hayafai kuendelea. 7. Dhambi Yaufikia Mwisho Wake Ingawa
Shetani na kundi lile kubwa sana lililosongamana la watu wale waovu
wanakiri kwamba njia ya Mungu haijabadilika, tabia zao bado zina dhambi.
Na baada ya hukumu ile kutamkwa wale waovu:
8. Dunia Inatakaswa Na Yafanywa Upya Kutoka
katika majivu yale ya maangamizi makuu ya mwisho, Mungu ataiumba dunia
mpya:
Je! wewe unapanga kuwa wapi siku hiyo? Je! umeamua kuwa pamoja na Kristo ndani ya mji ule na kuokolewa milele? Au utakuwa nje ya ule mji bila Kristo na kupotea milele? Kama
wewe umeyakabidhi maisha yako mikononi mwake Yesu, basi, huna haja ya
kuionja ile hofu isiyoneneka ya wale walio nje ya mji ambao wanatambua
kwamba wamepotea milele. Haidhuru maisha yakuletee kitu gani, kama wewe
unayaweka maisha yako mikononi mwake Yesu hivi sasa, basi, unaweza kuwa
ndani ya mji ule pamoja na Kristo na pamoja na wale waliokombolewa.
Endapo wewe hujafanya hivyo, basi mpe Yesu moyo wako sasa, naye atakuzungushia
upendo wake na msamaha. Hii ni nafasi yako ya pekee. Hii ndiyo siku
yako ya wokovu kwako.
© 2004 The
Voice of Prophecy Radio Broadcast |