SIRI YA MTINDO WA MAISHA ULETAO AFYA Watafiti wanaoishi katika kipindi hiki tulicho nacho wamejitahidi sana kuithibitisha ile kweli iliyothibitishwa kwanza na Biblia kwa kutoa maelezo haya: Wanadamu ni viumbe kamili. Mara nyingi kile tunachokigawa katika sehemu za kimwili, kiakili, na kiroho ni sehemu za mtu zilizo na uwiano unaoingiliana, wala hazitenganishiki. Kwa maneno mengine, kinachoidhuru akili, kinaudhuru mwili.Hali yetu ya kiroho ina shinikizo lake juu ya hali yetu ya kimwili, na kinyume chake. Sisi ni watu kamili. Kwa mfano watafiti wa kisayansi katika uchunguzi wao uliodhibitiwa wamegundua kwamba kicheko kile kitokanacho na furaha na shangwe huleta mabadiliko yanayoweza kupimwa katika mfumo wa kinga mwilini mwa mtu. Unaweza kabisa kuusaidia mwili wako kupigana na ugonjwa kwa vizuri zaidi ukiwa na furaha! Uchunguzi huo huonyesha jinsi akili na mwili vinavyofanya kazi yao kwa pamoja kwa ushirikiano wa karibu sana. Katika
maelfu ya miaka iliyopita Neno la Mungu lilidokeza kuwapo kwa uhusiano
huo wenye nguvu kati ya akili na mwili ambao ni hivi karibuni tu umekubaliwa
na kuingizwa katika nadharia ya kiganga: Kulingana
na mtume Yohana, Je, Ni kwa karibu jinsi gani uhusiano huo uliopo kati
ya akili na mwili unaathiri usitawi wetu wa kiroho? Muumbaji wetu anataka sisi tupate " kufurahia kuwa na afya njema " Neno la Mungu linaweza kutumika kama chemchem yetu ya afya, pamoja na kuwa chemchem yetu ya uzima wa milele. Kwa
kuwa usitawi wetu kimwili na kiakili na kiroho unakwenda bega kwa bega,
Paulo anatoa kwetu ombi hili: Injili inajumuisha mambo yote mawili, uponyaji wa mwili na uponyaji wa roho. Mtindo wa maisha uletao afya unaweza kutusaidia sisi kuwa Wakristo wenye uchangamfu mwingi. Hapa zipo kanuni nane za kufuata endapo wewe kweli unataka kuishi maisha yenye afya na yenye manufaa mengi zaidi. 1. Hewa Safi Hewa safi ya nje, ni ya lazima kwa afya nzuri. Wakati wa mchana na wakati wa kulala usiku, kuingiza na kuitoa hewa kwa njia inayofaa katika nyumba zetu na mahali petu pa kazi hutuhakikishia kwamba damu yetu daima itagawa oksijeni ya kutosha kila sehemu ya mwili wetu. Kuvuta pumzi nyingi wakati wa matembezi ya asubuhi ni njia kuu ya kuupatia mwili wako oksijeni. Aina ya hewa tuivutayo ni dhahiri kwamba ni ya maana. Jihadhari usikae mahali penye moshi au mvuke mwingi, penye hewa mbaya au hewa inayochukua vijimea vidogo sana (bacteria) kutoka mahali fulani palipojificha. Kuvuta tumbako huichafua sana hewa na ni mojawapo ya wauaji wakuu wa siku hizi. Utafiti wa sayansi umethibitisha kuwapo kwa uhusiano unaoleta madhara kati ya tumbako na kansa ya mapafu, ugonjwa wa kuvimba mapafu na kupumua kwa shida ( emphysema) na ugonjwa wa moyo. Mazoea ya mwili kuhusiana na hiyo sumu ya nikotini katika sigareti hufanya uvutaji huo wa sigara (tumbako) uwe mmojawapo wa mazoea magumu kabisa kuachana hayo. Kuvuta tumbako kutaweza kuwaua watu milioni 12 kwa mwaka kufukia mwaka wa 2020 endapo mwendo huu wa sasa utaendelea 2. Mwanga Wa Jua "Faida za mwanga wa jua ni nyingi: 1. Dakika kumi na tano hadi 30 za kupata mwanga wa jua kila siku katika ile sehemu ya mwanzo ya asubuhi au baadaye mchana alasiri husaidia mwili kukusanya pamoja au kutengeneza Vitamini D yake wenyewe, kirutubisho muhimu/homoni ndani ya ngozi. Vitamini D huisaidia damu kutengeneza kalisi (calcium) na fosforasi, inayoijenga na kuitengeneza mifupa. 2. Mwanga wa jua unafanya kazi yake kama dawa ya kuvika viini vya maradhi na kuua vijimea vidogo sana (bacteria) 3. Jua linatoa nguvu ambayo kwa hiyo mimea inaweza kuigeuza kaboni dioksidi na maji kuwa kabohidreti [chakula cha wanga] Bila ya njia hiyo wanyama na wanadamu wangekufa kwa njaa 4. Jua pia linamsaidia mwanadamu kujirekebisha na kukabiliana na kazi ya usiku na kupunguza unyong'onyevu (depression) unaotokana na siku za giza wakati majira ya baridi kali yanapotokea. Neno la tahadhari: Mwanga wa jua unaweza pia kuleta madhara kukaa kwa muda mrefu kwenye mwanga wa jua kunaweza kuiunguza ngozi, kunaweza kuongeza hatari ya kupatwa na kansa ya ngozi kunaweza kuharakisha kuzeeka, kunaweza kuyaharibu macho, na kusababisha mtoto wa jicho (cataracts). " [Madondoo yote katika Mwongozo huu yamenukuliwa kutoka katika Look up and Live: A Guide to Health, Lesoni ya Watu Wazima, Robo ya kwanza ya mwaka wa 1993, (Nampa, Idaho: Pacific Prexss Publishing Association). Mambo mengi katika Mwongozo huu ambayo hayajawekwa katika Alama za kunukuu yamefundishwa kutoka katika lesoni hiyo hiyo] 3. Kupumzika Mwili huu ni lazima upumzike ili upate kujitengeneza upya wenyewe. Yatupasa kuwa na muda wa burudani na wa kupumzika ili kupunguza msongo utokanao na kazi pamoja na majukumu ya kifamilia. Bila kuwa na muda wa kutosha kupumzika mara nyingi watu wanakuwa na wasiwasi, mfadhaiko na hasira kali. Msongo huo wa moyo unaweza kuleta ugonjwa ambao utatulazimisha kuchukua pumziko letu ambalo miili yetu ilikuwa inataka kwa muda wote. Hakuna kitu cha badala cha kuweka mahali pa usingizi mzuri wa usiku. Kuzichaji upya betri zetu za kiroho kwa kuweka utaratibu wa kila siku ni muhimu pia kwa afya yetu ya kimwili. Muda wa kila siku anaotumia Mkristo katika kutafakari, kusoma Biblia, na maombi utaweza kuuponya mwili pamoja na roho. Tunakuhitaji pia kupata pumziko ili kuuvunja mzunguko wa kazi, yaani, kuwa na siku ya kupumzika kila juma, na likizo ya mwaka au nusu mwaka. 4. Mazoezi Ya Mwili Mazoezi
ya mwili ni ya muhimu sana kwa afya yetu: Endapo wewe ulikuwa hufanyi mazoezi, basi anza taratibu (polepole) na kuongeza nguvu yake hatua kwa hatua upatapo uwezo wa kustahimili. Laweza kuwa ni jambo la busara kumwona mganga wako kabla ya kuanza mazoezi hayo. Lengo lako na liwe kujishughulisha na kila aina ya mazoezi hayo ya mwili ambayo yanaweza kulinganishwa na kutembea maili moja kwa dakika kumi na tano mara nne au zaidi kw ajuma. 5. Maji Kwa
vile maji ni ya lazima kwa kila seli mwilini, basi, ingetupasa kunywa
maji mengi. 6. Lishe Ifaayo Wakati
ule wa uumbaji Mungu alimwagiza Adamu na Hawa kula chakula cha kokwa,
nafaka na matunda (Mwanzo 1:29). Baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi,
ziliongezwa mboga za majani katika lishe yao Nyama ya wanyama ina mafuta ya majimaji (saturated fat) na mafuta mazito kolestero [cholesterol], ambayo yote huongeza hatari ya kupatwa na shinikizo la damu, kupooza (stroke), ugonjwa wa moyo, kansa, unene usio wa kawaida, kisukari na magonjwa mengineyo. Leo matabibu wengi wanawashauri wale wanaokula nyama kula mnofu ule tu usiokuwa na mafuta, uliopikwa vizuri, pamoja na kula samaki na kufanya hivyo kwa nadra sana. Kwa vile watu wanaokula chakula cha mimea wana afya bora zaidi, tena wanaishi kwa muda mrefu zaidi, wataalamu wengi wa lishe na afya wanatusihi sana sisi ili tupate kufikiria kukirudia chakula kile cha awali walichopewa wanadamu cha kokwa, nafaka na matunda pamoja na mboga za majani zilizoongezwa. Ukitaka kuanza kula vyakula vya mimea, hakikisha kwamba unaelewa kwanza namna ya kuandaa lishe bora bila kutumia nyama. Ule kiasi cha chakula kinachomtosha mtu kula kwa siku (migawo [serving] mitano au sita hivi) ya aina mbalimbali za matunda, pamoja na kokwa [karanga n.k.] nafaka, maharage, kunde, mbaazi na mboga za majani. Mboga za majani za kijani na za njano, pamoja na machungwa ni za muhimu sana. Tumia unga wa nafaka isiyokobolewa na mchele mwekundu (brown rice) badala ya ule mweupe. Ulaji wako wa wanga na sukari za mchanganyiko ungekuwa katika migawo (servings) sita au zaidi kwa siku moja. Badilisha matumizi yako ya mafuta ya wanyama (samli, siagi, mafuta ya nguruwe, shahamu izungukayo figo, n.k.) kwa kutumia mafuta ya mimea. Lishe hiyo juu inatosha bila kutumia nyama kama wewe unatumia vitu vinavyotokana na maziwa. Wale wanaochagua kula nyama kama sehemu ya chakula chao, wangepaswa kuzila nyama zile tu ambazo Biblia inasema ni "safi"au zile zinazofaa kuliwa na wanadamu. Mungu alipowaruhusu wanadamu kula nyama baada ya gharika (Mwanzo 7:2-3) (Mambo ya walaei 14:47), alibainisha nyama za wanyama gani zilikuwa safi, na zipi zilikuwa najisi na zilikuwa hazifai kuliwa. Soma katika Mambo ya Walawi 11 na Kumbukumbu la Torati 14 orodha ya ndege, wanyama, na samaki ambao Mungu alisema hawafai kuliwa. Kwa mujibu wa sura hizo, wanyama safi ni lazima kwato zao zigawanyike na pia wacheue. Samaki safi ni lazima wawe na magamba na mapezi, vyote viwili. Ndege wanaokula uchafu ni marufuku kuliwa. Miongoni mwa wanyama najisi, kwa namna ya pekee nguruwe wanatajwa kwa kulaaniwa (Kumbukumbu la Torati 14:8) Asilimia ya juu ya miili ya wanadamu inayofanyiwa uchunguzi na waganga imejaa minyoo isiyokufa ya trikina (trichinae). Minyoo hiyo midogo sana inahamishiwa kwa wanadamu wale wanaokula nguruwe walioambukizwa minyoo hiyo. Utafiti wa kisanyansi wa siku hizi unazidi kufunua sababu zinazoonyesha kwa nini Mungu alitangaza nyama za wanyama fulani kuwa ni najisi. Sababu moja huenda ikawa ni yale matokeo yanayoleta uharibifu mkubwa kutokana na mafuta ya wanyama ya majimaji katika mfumo wa mwili wa kibinadamu wa kuyeyusha chakula. 7. Epuka Vitu Vinavyoleta Madhara Je,
ni maonyo gani ambayo Biblia inatoa kuhusu vinywaji vyenye alcohol ndani
yake? Wala wezi wala watamanio, wala WALEVI, wala watukanaji hawataurithi ufalme wa Mungu" - (1 Wakorontho 6:10). Alkoholi
huathiri mifumo ya mwili ifuatayo: Alkoholi inahusika na asilimia kubwa ya watu wanaojiua wenyewe, vifo vinavyosababishwa na magari, kuwatendea vibaya watoto, na ukatili uliomo nyumbani. 8.
Kuutumainia Uweza Wa Mungu "Ee nafsi yangu umhimidi BWANA, wala usizisahau fadhili zake zote - yeye anayekusamehe dhambi zako zote na KUKUPONYA MAGONJWA YAKO YOTE, ANAYEUKOMBOA UHAI WAKO na kaburi" - Zaburi 103:2-4. David Larson, mshauri wa Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akiliki kule Marekani, alifanya utafiti wake mpana juu ya uhusiano wa moja kwa moja uliopo kati ya dini na afya.Uchunguzi wake ulionyesha wazi kwamba upo uhusiano wa moja kwa moja kati ya Mkristo aliyejitoa na afya. Alishangaa kujua kwamba, wale wanaohudhuria kanisani wanaishi kwa muda mrefu kuliko wale wasiohudhuria. Wale wanaokwenda kanisani wana upungufu wa kupatwa na mshtuko wa moyo, Mishipa ya arteri kuwa migumu, shinikizo la damu, na magonjwa mengine. Wale wanaomwamini Mungu huishi maisha yenye manufaa zaidi kwa sababu hawapatwi kirahisi na mfadhaiko, hawageuki na kuwa walevi sugu, kufungwa kama wahalifu wanaorudia mle tena na tena, na kunaswa katika ndoa isiyo na furaha. Kuutamainia uweza wa Mungu ndio msingi wa ustawi wa kweli na maisha ya afya yenye furaha. Waadventista,
Wasabato wapatao 50,000 hivi walichunguzwa, hasa kule California kwa
kipindi cha zaidi ya miaka 30. Matokeo yalionyesha kwamba Waadventista
wanaume wanaishi miaka 8.9 na wanawake miaka 7.5 kuliko Tukiutumia mtazamo wa Biblia katika maisha yetu tutakuwa tofauti katika aina zote za njia za utendaji wetu na kutoa ushahidi unaovutia kuonyesha kwamba katika ulimwengu mzima Ukristo ni dini inayoweza kuwekwa katika vitendo. Inawabadilisha watu - yaani, fikra zao na matendo yao na kujenga mtindo mpya wa maisha. Kutokana na uhusiano wa karibu sana uliopo kati ya akili, mwili na maisha yetu ya kiroho, Wakristo wale wanaoishi kwa Neno la Mungu watataka kuzifuata kanuni hizo za mtindo wa maisha uletao afya wanapojiandaa kwa ajili ya marejeo yake Yesu (1 Yohana 3: 1-3). Sio tu kwamba Kristo anataka sisi tuwe tayari kukutana naye atakaporudi, pia anataka kuyaboresha maisha yetu ya sasa. Tunaweza kushirikiana naye kwa kuzifuata hizo kanuni za afya za Mungu. Yesu
anaahidi kutuokoa sisi mbali na kila tabia iletayo uharibifu mwilini
kwa " kadri ya nguvu [yake] itendayo kazi ndani yetu" (Waefeso
3:20). Endapo wewe unajitahidi kuishinda tabia fulani inayokuathiri
mwili wako kama vile kutumia tumbaku au kunywa vileo, basi, maazimio
yako hayo mazuri sana ya kutaka kuacha tabia hiyo mara nyingi yanageuka
na kuwa kwako kama kamba za mchanga. Lakini kwa kuuchota uwezo wa Mungu
unaotenda kazi ndani yako Mungu aweze kukupa wewe nguvu za kukuwezesha
kushinda. Neno la Mungu linaahidi hivi: " Naweza kufanya mambo
yote kwa njia yake Kristo anitiaye nguvu" (Wafilipi 4:13)
© 2004 The
Voice of Prophecy Radio Broadcast | |