MPANGO KWA AJILI YA MAISHA YAKO Baada ya mchungaji kuzungumza juu ya somo hili, "Kwa nini mimi namwamini Yesu," mwanaume mmoja kijana, aliyevalia vizuri, alimtembelea katika chumba chake cha kusomea na kusema naye kwa mshangao, "Hotuba yako usiku wa leo ilitoka katika Biblia yako. Hebu niambie, kama Yesu alipata kuishi hapa duniani, mbona historia haisemi habari zo zote juu yake? "Hilo ni swali zuri," mchungaji akajibu alipogeuka na kuchukua vitabu kadhaa na kuviweka chini. "Lakini, kwa kweli, historia inasimulia habari za Yesu Kristo." "Hizo ningependa kujionea mwenyewe," yule mwanaume kijana akajibu. "Vema, hapa ni barua ya 97 ya kitabu cha 10 cha barua za (Pliny) Ndogo, Balozi wa Roma katika nchi ya Bithinia, jimbo la Asia ndogo ya zamani. Plinio alimwandikia mfalme wa Dola ya Roma Trajani (Trajan), akimwambia habari za matukio katika jimbo lake. Tazama, hapa anaomba ushauri juu ya jinsi anavyopaswa kulishughulikia dhehebu jipya, yaani, Wakristo. Anasimulia habari inayohusu kuongezeka kwao haraka sana na jinsi walivyoimba nyimbo za kumsifu Mungu zilizotungwa kwaajili ya kiongozi wao, yaani, Kristo. Pliny aliituma barua yake karibu na mwaka ule wa 110 B.K. Barua hiyo iliyoandikwa na Pliny inatoa ushahidi wa kihistoria wa yule mwanadamu, Kristo, na juu ya kuenezwa kwa imani yake katika siku zile za mitume wake." Akiwa ameshangaa, mwanaume yule kijana alisema, "Hebu niambie zaidi!" Mchungaji
alipoendelea kukipekua kitabu kingine, aliongeza kusema hivi, "Mwanahistoria
mwingine, aliyeishi kipindi kile kile kimoja na Pliny, alikuwa ni Tacitus.
Katika habari zake za miaka zilizotengwa (Anals), kitabu cha 15, sura
ya 44, anasimulia habari za uhasama aliokuwa nao Nero na mateso yake
dhidi ya Wakristo wakati mji wa Roma ulipochomwa moto. Tacitus anaeleza
kwamba neno hilo "Mkristo" linatokana na jina la 'Kristo.'
Anataja kwamba Yesu Kristo, mwasisi wa dini ya Kikristo, alikuwa ameuawa
na Pontio Pilato wakili wa Yudea, katika kipindi cha utawala wa mfalme
wa Dola Tiberio. Maelezo haya yote anayotupa Tacitus yanalandana kabisa
na matukio, majina na mahali palipotajwa katika Biblia." Mchungaji
yule akaongeza kusema hivi, "Nataka uzingatie kwamba karibu na
mwaka wa 180 B.K. Celsus aliandika kitabu akiwashambulia Wakristo, akionyesha
kwamba kufikia wakati ule Ukristo ulikuwa ni nguvu iliyopaswa kutambuliwa. Yule mwanaume kijana alipotambua kwamba historia zote mbili, yaani, ile takatifu na ile ya kidunia, zinakubaliana kwamba Yesu alipata kuishi hapa duniani kama mwanadamu, alikwenda zake akiwa ameamini kwamba Yesu Kristo alikuwa mtu halisi wa kihistoria. 1. Kristo Alikuwako Tangu Milele Yesu
hakuwa tu mtu mwema, alikuwa Mungu pia. Je, ni madai gani aliyoyatoa
Yesu mwenyewe kuhusu Uungu wake? Ukitaka kujua jibu kwa maswali haya, "Mungu ni nani? Anafananaje?" unapaswa kumtazama tu Yesu, aliyetangaza, akasema, "Mimi na Baba Tu umoja (Yohana 10:30.) Mungu Baba na Yesu mwanawe wamekuokoa pamoja tangu milele (Waebrania 1:8.) Haukuwako wakati wo wote ule ambapo Kristo hakuwa umoja na baba yake. Baba yake anatoa upendo na ulinzi wake ule ule kwa kila mtu kama aliouonyesha Yesu katika kipindi cha maisha yake ya kibinadamu hapo duniani. 2. Kristo, Kiini Cha Historia Na Unabii Kwa
kuwa kisa cha maisha ya Kristo ni utimizo wa unabii, kisa cha maisha
yake kiliandikwa kabla yeye hajazaliwa unabii wa Agano la kale huonyesha
kwa kifupi kinachoeleweka wazi maisha yake, kifo chake na ufufuo wake
kabla hayajatokea. Agano Jipya ni kisa cha maisha yake kilichoelezwa
kama utimilizo wake. Wakiishi kuanzia miaka mia tano hadi elfu moja
na mia tano kabla ya kuzaliwa kwake Kristo, manabii wale wa Agano la
Kale waliotoa utabiri mwingi wa pekee kuhusu maisha yake Masihi, na
tangu mwanzo kabisa wa kazi yake hapo duniani, Mwokozi
wetu aliwaelekeza watu kwenye unabii uliotimizwa ili kuthibitisha kwamba
yeye ndiye: Unabii uliotimizwa unatoa ushahidi unaosadikisha kwamba Yesu ndiye yule Masihi aliyeahidiwa. 3. Maisha Ya Kristo Ni Utimilizo Wa Unabii Hebu na tuviangalie vifungu hivi vichache vya unabii huo toka katika Agano la Kale - na kutimizwa kwake katika kumbukumbu za Agano Jipya. Mahali
Pake Alipozaliwa Kuzaliwa
Kwake Na Bikira UKOO
WAKE WATOKA KATIKA KABILA LA YUDA,... mpaka atakapokuja yeye anayeimiliki"
- (Mwanzo 49:10). Kukataliwa
Kwake Kusalitiwa
Kwake Na Ujira Aliolipwa Msaliti Wake Kifo
Chake Msalabani Kutoka
Kwake Kaburini Baada ya kuuangalia ushahidi huo, tunahitaji kufanya uamuzi wetu kwa njia ya maombi kuhusu nani atakayekuwa Bwana katika maisha yetu. Kama wewe bado hujafanya hivyo, je! utayaweka maisha yako mikononi mwake Yesu? 4. Maisha Yaliyopangwa Na Mungu Yesu
aliishi maisha yaliyopangwa na Mungu, ambayo yameelezwa kwa maelezo
machache mamia ya miaka kabla ya kuzaliwa kwake. Siku zote akiwa anautambua
ukweli huo, alikuwa mwepesi kutambua maongozi ya Mungu. Kristo alisema: Mungu alipanga maisha ya kibinadamu ya Yesu kabla ya kuzaliwa kwake, tena Mungu anao mpango kwa kila mwanadamu pia. Anajua jinsi kila mmoja wetu anavyoweza kutimiza haja zake zenye kina sana na kujipatia maisha tele. Ray siku zote hakuwa na hakika kabisa iwapo alitaka kuufuata mpango wa Mungu. Lakini alipokabiliwa na uamuzi mkubwa kuhusu wapi alipaswa kwenda kusoma chuoni, basi, kwa mara yake ya kwanza katika maisha yake aliamua kutafuta uongozi wa Mungu katika suala lile. Aliomba kwa siku kadhaa na kujitahidi kusikiliza jibu la aina fulani. Baada ya muda fulani kupita alionekana amepata sababu zilizo wazi sana kwa nini angepaswa kuchagua chuo B: Chuo Kikuu kisicho na gharama kubwa sana, lakini kikubwa na ambacho hakiendeshwi na mtu fulani mahsusi. Mara tu baada ya kuanza kusoma pale alifahamiana na Wakristo fulani wa ajabu waliokuwa wamejiunga na chama fulani cha kumtetea Kristo katika eneo lile la kile chuo kikuu. Uzoefu wote aliokuwa nao pamoja nao katika kipindi cha miaka miwili iliyofuata uliyabadilisha maisha yake kabisa. Ray anapoangalia nyuma leo, anaona kwamba kila wakati alipokuwa amekabiliwa na uamuzi mkubwa na kutafuta uongozi wa Mungu, "Mungu alinifunulia uwanja mpya wa maisha yangu." Je, unawezaje kuujua mpango wa Mungu kwa maisha yako? Mungu anatoa uongozi wake kwa njia kadhaa: 1.
Biblia 2.
Maongozi Ya Mungu Katika Mambo Yanayotupata 3.
Mawasiliano Toka Kwa Mungu Ya Moja Kwa Moja hadi Moyoni 1:18). Kadiri tunavyozidi kufanya mazoezi ya kuwasiliana na Mungu ndivyo kadiri anavyoweza kutuongoza sisi. Anaziumba upya hisia zetu za ndani na uwezo wetu wa kufikiri na kuamua ili tupate kuiona wazi hatua inayaofuata ambayo tunahitaji kuichukua. 5. Maongozi Hayo Ni Lazima (Yapatane)? Naam, yawezekana kudhani kwamba wewe unaishi maisha yanayoongozwa na Mungu wakati wewe unafuata tu mielekeo yako na hisia zako mwenye (Mithali 16:25). Hisia zetu ni lazima zipatane na mafundisho ya Biblia. Si salama kuamua kwamba ni Mungu anayetuongoza isipokuwa kama maongozi yote matatu yanapatana. Hebu na tumchukue Jake, kwa mfano. Alikuwa na mke wake mzuri sana na watoto wawili, lakini alifanya uzinzi na mwanamke mwingine. Aliwaambia hivi rafiki zake: P "Mimi nimeliombea jambo hilo, nami najua kwamba hayo ni mapenzi ya Mungu." Hisia za moyoni za Jake na "maono yake ya ndani" kwa dhahiri yalimpeleka katika njia ile mbaya iliyokwenda chini. Yeye aliwaza kwamba yale yalikuwa ni "maongozi ya Mungu"yaliyompelekea kukutana na mwanamke yule mwingine, wala hakurudi nyuma kuziangalia amri za Biblia dhidi ya uzinzi. Na Biblia hiyo, ambayo ni "sheria na ushuhuda," ndicho kitabu cha mwongozo chenye mamlaka, ndiye mwamuzi wa mwisho anayeamua njia sahihi ya kufuata katika utendaji wetu (Isaya 8:20). Kamwe tusiruhusu maoni yo yote au jambo lo lote linaloonekana wazi kuwa ni maongozi ya Mungu kutupeleka mbali na kanuni ya Biblia. 6. Kujikabidhi kwa Mpango Wa Mungu Shetani
alipokuja kumjaribu Yesu kule nyikani, alitoa shauri hili, "Kama
wewe ukiachilia mbali kujitoa kwako mhanga kunakokuletea maumivu Fundisho moja lenye nguvu tuwezalo kujifunza kutokana na maisha yake Yesu ni utii wake kwa mapenzi ya Baba yake. Hata katikati ya maumivu makali ya kutisha ya Gethsemane, yeye akalia, kasema, "Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke. Walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe" (Mathayo 26:39). Baada ya ile miaka mitatu ya kazi yake, akiishi siku kwa siku kupatana na mpango wa Baba yake, Kristo alipokuwa akifa maneno yake yalikuwa ni haya: "Imekwisha" (Yohana 19:30). Yesu alikuwa akisema maneno haya hasa, "maisha yangu yaliyopangwa na Mungu sasa yamekamilika na kutimilika." Unapoanza
kuisikia Sauti ya Mungu ikisema nawe kulingana na Neno lake, kupitia
katika mambo yale yakupatayo yanayoongozwa na Mungu, na kupitia katika
mawazo ya moja kwa moja, unaweza kujifunza kuyakubali maongozi yake
hayo kwa moyo wako wote. Wewe pia waweza kuigundua furaha ya maisha
yaliyopangwa na kuongozwa na Mungu.
© 2004 The
Voice of Prophecy Radio Broadcast | |